Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA LA FIFA QATAR 2022:Ufaransa yafanikiwa kuingia fainali baada ya kuifunga Morocco bao 2-0

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la dunia kwa mara nyingine tena baada ya kuifunga timu ya Morocco bao 2-0 katika uwanja wa Al Bayt Doha Qatar.

Mchezaji Theo Hernandez alifunga bao la kwanza katika dakika ya 5 ya mchezo na kuwafanya Morocco kuwa nyuma mapema kabisa katika mchezo huo naye mshambuliaji Randal Kolo Muani alipachika bao la pili na kufunga kitabu cha magoli katika dakika ya 79 ya mchezo na kufuta matumaini ya Morocco kucheza fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Timu ya Ufaransa ilitiwa moyo na kucheza kwa kujituma mbele ya Rais wao Emmanuel Macron ambaye alikwenda uwanjani kushuhudia mchezo huo.

Pamoja na Morocco kutafuta nafasi nyingi, mbinu za Ufaransa za kukabiliana na mashambulizi zilizidi kuwa hatari zaidi. Kombora la Kylian Mbappe katika dakika ya 35 lilimpita Bounou na kuondolewa nje ya mstari, huku kutoka umbali mrefu Giroud akipiga shuti kali lakini likaenda nje ya lango lisilo na ulinzi katika sekunde zilizofuata.

Morocco waliamka katika dakika za mwisho za mchezo huo na kukosa nafasi za wazi katika dakika ya 75 na 77 ambazo kama wangetumia vyema pengine mambo yangebadilika kwa upande wao.

Hata hivyo Morocco, bado wameweka alama ya juu kwa bara la Afrika na ulimwengu wa Kiarabu, na bado watakuwa na mchezo wa kugombea nafasi ya tatu Jumamosi dhidi ya Croatia.

Kwa upande mwingine, Ufaransa itajaribu kutetea taji lao la Kombe la Dunia na kumaliza ndoto tofauti, huku Leo Messi na Argentina nao wakijaribu kutimiza ndoto ya Messi kuinua kombe la dunia hasa akiwa amekwishatangaza kuwa mchezo wa Jumapili ndio wa mwisho kwake kuchezea timu yake ya taifa.

Post a Comment

0 Comments