Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Korea Kusini Kukutana na Brazil Hatua Ya 16-Bora Baada Ya Kulaza Ureno Katika Kundi H

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

HWANG Hee-chan alifungia Korea Kusini bao la dakika za mwisho katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Ureno na hivyo kuwapiga kumbo Uruguay kwa wingi wa mabao katika Kundi H na kufuzu kwa hatua ya 16-bora ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Hwang alicheka na nyavu za Ureno katika dakika ya 91 baada ya kukamilisha krosi safi kutoka kwa Son Heung-min.

Korea Kusini walishuka dimbani wakihitaji ushindi wa mabao mengi ili kuweka hai matumaini ya kuungana na Ureno ambao tayari walikuwa wamejikatia tiketi ya raundi ya 16-bora baada ya kushinda Ghana (3-2) na Uruguay (2-0) katika michuano miwili ya kwanza ya Kundi H.

Uruguay waliotandika Ghana 2-0 ugani Education City, walihitajika kufunga Ghana zaidi ya mabao mawili ili kuwapiku Korea Kusini ambao pia walikamilisha kampeni za makundi kwa alama nne, moja kuliko Ghana na mbili nyuma ya Ureno.

Ureno sasa watavaana na Uswisi katika hatua ya 16-bora huku zawadi kwa Korea Kusini kwa kumaliza wa pili katika Kundi H ikiwa ni kumenyana na Brazil – mabingwa mara tano wa dunia waliotamalaki Kundi G kwa alama sita baada ya kuwalemea Uswisi kwa wingi wa mabao.

Post a Comment

0 Comments