Ticker

6/recent/ticker-posts

Kombe la Dunia FIFA 2022: Japan Yaitandika Uhispania

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Katika sinema inayoendelea kushuhudiwa katika mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar, Japan imeifunga Uhispania katika mechi ya mwisho ya kundi E. 

Japan ambayo ilipoteza mechi yake ya pili katika kundi E kwa kutandikwa 1-0 na Costa Rica imetoka nyuma na kufanikiwa kushinda 2-1 dhidi ya Uhispania. 

Alvaro Morata aliipa Spain uongozi katika dakika ya 11 ya mchezo na kuchochea sherehe katika kambi ya Ujerumani kwani mambo yalikuwa yanaenda walivyotamani. 

Hata hivyo  Tanaka na Ritsu Doan walicheka na nyavu katika kipindi cha pili na kuipa Japan ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa wa mwaka 2010. 


Japan yaongoza kundi E katika Kombe la Dunia nchini Qatar 

Japan vilevile ilitoka nyuma na kufanikiwa kushinda 2-1 dhidi ya Ujerumani katika mechi yao ya ufunguzi katika kundi E. 

Kwa kupoteza mechi dhidi ya Costa Rica na kushinda dhidi ya miamba wengine Uhispania, timu hiyo ya Bara Asia imejikakikishia uongozi wa kundi E kwa alama sita. 

Uhispania imekuwa ya pili kwa alama nne na ubora wa mabao huku Ujerumani na Costa Rica zikiondoka katika nafasi ya tatu na nne. 

Post a Comment

0 Comments