Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Argentina Watinga Hatua Ya 16-Bora

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

ARGENTINA wamefuzu hatua ya 16-bora ya Kombe la Dunia mwaka huu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Poland katika mchezo wa mwisho wa Kundi C katika uwanja wa 974, Qatar.

Licha ya kulazwa na Argentina, Poland bado walifaulu kutinga hatua ya mtoano kwa wingi wa mabao ikizingatiwa kuwa walijizolea alama nne sawa na Mexico walioizamisha Saudi Arabia 2-1 katika mchezo mwingine wa Kundi C uwanjani Lusail Iconic.

Lionel Messi alichochea ushindi muhimu wa 2-0 uliosajiliwa na Argentina dhidi ya Mexico mnamo Novemba 26, 2022 baada ya kufungua kampeni zao za makundi kwa kichapo cha 2-1 dhidi ya Saudi Arabia.

Argentina wanaopigiwa upatu wa kunyanyua Kombe la Dunia mwaka huu, sasa watakutana na Australia katika raundi ya 16-bora ugani Ahmad Bin Ali mnamo Disemba 3, 2022.

Poland ambao wangefuzu kwa uchache wa kadi za manjano iwapo Saudia Arabia wangetoka sare na Mexico, sasa watamenyana na Ufaransa katika raundi ya 16-bora mnamo Disemba 4, 2022 uwanjani Al Thumama.

Kombe la Dunia ndilo taji la pekee ambalo Messi hajawahi kunyanyua katika taaluma yake ya soka.

Fainali za mwaka huu ni za tano kwa Messi na za mwisho kwa supastaa huyo wa Paris Saint-Germain (PSG) akivalia jezi za Argentina. 

Argentina waliotawazwa mabingwa wa dunia mnamo 1978 na 1986, walitwaa taji la Copa America kwa mara ya kwanza tangu 1993 mnamo Julai 2021 na wakafuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar bila kushindwa. Waliambulia nafasi ya pili kwenye Kombe la Dunia mnamo 1990 na 2014.

Post a Comment

0 Comments