Ticker

6/recent/ticker-posts

Gabriel Martinelli akaribia kukubali mkataba mpya Arsenal

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

NYOTA wa Arsenal, Gabriel Martinelli, anakaribia kukubali mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo baada ya mazungumzo sasa kuwa katika hatua ya mwisho, kulingana na mchambuzi wa masuala ya uhamisho, Fabrizio Romano. Mkataba wa Mbrazil huyo unamalizika Juni 2024,Lakini 'The Gunners' wanataka kumbakisha klabuni hapo. 


Martinelli aliwasili katika kikosi hicho cha London Kaskazini mwaka 2019 akitokea Ituano ya Brazil na amekuwa mchezaji muhimu tangu wakati huo, akicheza mechi 104 na kuchangia mabao 38. Alishinda Kombe la FA katika msimu wake wa kwanza.


Bado haijakamilika au kukubaliwa kikamilifu, pia hakuna kilichosainiwa - lakini inakaribia.


Romano amesema mkataba huo mpya haujakamilika au kukubaliwa bado, na hakuna chochote ambacho kimetiwa saini, lakini pande zote mbili zinakaribia kumalizana. Aliongeza kuwa Bukayo Saka na William Saliba ni vipaumbele kwa Arsenal pia katika suala la kusaini mkataba mpya, na wachezaji wote wawili wamekuwa kivutio msimu huu.


Akiwa na mabao manne na asisti sita, Saka amekuwa na mabao mengi zaidi kikosini nyuma ya Gabriel Jesus pekee huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, akiibuka kinara katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal.


Liverpool Waizidi Ujanja Man Utd kwa cody gakpoPost a Comment

0 Comments