Ticker

6/recent/ticker-posts

EPL Kurejea Hii Leo Baada ya Wiki Sita, Arsenal kuwakaribisha West Ham

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Mechi za Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama EPL zinarejea hii leo baada ya likizo ya wiki sita huku ratiba ya ligi hiyo ikiwa imeshona vya kutosha katika wiki kadhaa zijazo. 


EPL kama tu ligi zingine kuu duniani kote zilichukua mapumziko mwezi Novemba ili kupisha michuano ya Kombe la Dunia iliyoandaliwa nchini Qatar. 


Ligi hii inarejea Jumatatu - Disemba 26 - ikiwa ni Boxing Day na kuna mengi ya kupiganiwa kileleni na mkiani mwa msimamo wa EPL.

Vita Ya kileleni 


Viongozi Arsenal watakuwa wenyweji wa West Ham katika dimba la Emirates wakilenga kulinda pengo lao la alama tano kati yao na mabingwa watetezi Manchester City.


City ambao wanashikilia nafasi ya pili huenda wakajikuta alama nane nyuma ya viongozi kabla ya kuingia uwanjani kuchuana na Leeds United katika dimba la Elland Road mnamo Jumatano. 


Mbio za Champions League 


Mbio za kufuzu michuano ya klabu bingwa pia zitashuhudiwa Boxing Day zikihusisha Tottenham, Newcastle, Liverpool na Chelsea ambao wanashikilia nafasi ya tatu, nne, tano, sita na nane.


Klabu hizo nne zitachuana na Brentford, Leicester City, Aston Villa na Bournemouth katika usanjari huo mnamo Jumatatu. 


Manchester United inayoshikilia nafasi ya tano itachuana na Nottingham Forest mnamo Jumanne ili kupunguza pengo la pointi kati yake Tottenham. 


Nottingham kwa sasa inashikilia nafasi ya 18 kwenye msimamo wa EPL ikiwa na alama 13 baada ya mechi 15 lakini sio mechi rahisi kwa vijana wa Erik Ten Hag. 

Tetesi za Soka barani Ulaya Jumatatu 26.12.2022Post a Comment

0 Comments