Ticker

6/recent/ticker-posts

Claudio Ranieri Arejea Italia Kuwa Kocha Wa Klabu Ya Cagliari Baada ya Kukinoa Zaidi Ya Miaka 30 Iliyopita

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

CLAUDIO Ranieri ameaajiriwa tena kuwa kocha Wa Klabu Ya Cagliari, zaidi ya miaka 30 tangu apewe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kwa mara ya kwanza.


Umaarufu katika ulingo wa ukufunzi ulianza kumwandama akiwa kocha wa Cagliari kati ya 1988 na 1991 ambapo alifaulu kuongoza klabu hiyo kupanda ngazi kutoka Serie C hadi Serie A.


Ranieri, 71, ametia saini mkataba wa kunoa Cagliari hadi 2025, hiyo ikiwa ni kazi yake ya kwanza tangu atimuliwe na Watford mnamo Januari 2022.


“Narejea Cagliari – kikosi ambacho nimekijua kwa muda mrefu. Hata nilipoagana nacho 1991, niliahidi wadau wa klabu hiyo kwamba ningerudi baadaye kuwa sehemu ya shughuli,” akasema mkufunzi huyo raia wa Italia.


Ranieri anajaza pengo lililo achwa wazi na kocha Fabio Liverani aliye timuliwa na Cagliari mwanzoni mwa wiki hii baada ya matokeo duni yaliyoacha kikosi hicho katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa  Serie B.


Ranieri alitimuliwa na Watford mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 baada ya kuhudumu kambini mwa kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa kipindi kisichozidi miezi minne.


Aliwahi kukiongoza kikosi cha Leicester City kutwaa Ubingwa wa EPL mnamo 2015-2016 baada ya kuwa kocha wa Chelsea na Fulham.


Post a Comment

0 Comments