Ticker

6/recent/ticker-posts

Arteta Afichua Mipango ya Arsenal Kusajili Wachezaji Januari

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amezungumzia mipango ya klabu hiyo katika dirisha fupi la Uhamisho la mwezi Janauri. 


Kwa mujibu wa Arteta, klabu hiyo inalenga kufanya sajili zake mapema iwezekanavyo jinsi ilivyofanya katika dirisha la uhamisho lililopita. 


Tunataka kusajili mapema wachezaji katika dirisha la uhamisho la Januari kama tulivyofanya katika dirisha lililopita. Kile ambacho hatuwezi kuthubutu ni kuleta mchezaji ambaye hatatufaa, Arteta amesema. 


Arsenal kwa sasa inaongoza jedwali kwa pengo la alama tano ikiwa inawinda taji la kwanza la Ligi Kuu ya Uingereza tangu mwaka wa 2004.


Mwezi wa Januari ni muhimu sana katika safari yao kwani wana mechi dhidi ya Newcastle, Tottenham na Manchester United. 


Tulijua umuhimu wa kupata wachezaji mapema katika dirisha la uhamisho lililopita na tunataka kufanya vivyo hivyo mwezi Januari. Huo ndio mpango lakini wakati mwingine haiwezekani. Lakini ukiniuliza usemi wangu, tunawakata wachezaji haraka iwezekanvyo ili waingiliane na wenzao haraka, Arteta amesema. 


Arsenal wanarejea uwanjani Jumatatu - Disemba 26 - wakiwa na kibarua dhidi ya West Ham ugani Emirates katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza.


EPL Kurejea Hii Leo Baada ya Wiki Sita, Arsenal kuwakaribisha West Ham


Post a Comment

0 Comments