Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal 3-1 West Ham United, Arsenal yajikita kileleni mwa Premier League kwa tofauti ya Alama Saba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Klabu ya Arsenal imezidi kujiimarisha katika mbao za kuwania taji la Ligi kuu ya Uingereza(Premier League) baada ya kufanikiwa kuifunga  West Ham United mabao 3-1 katika dimba la Emirates hapo jana na kufanikiwa kuweka pengo la alama saba kileleni mwa msimamo. 


Arsenal ambao walielekea katika mechi hiyo wakiwa na pengo la alama tano kileleni mwa EPL, walitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya vijana wa David Moyes ambaye alikuwa kocha wa Mikel Arteta akichezea Everton. 


Simulizi ya mabao kwa mukhtasari 

Wageni West Ham ndio waliokuwa wa kwanza kucheka na nyavu baada ya kupata penalti iliyo fungwa na Said Benrahma katika dakika ya 27 baada ya beki wa Arsenal William Saliba kumdondosha Jarrod Bowen kwenye eneo la hatari. 


Arsenal walishindwa kupata goli katika kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili. 


The Gunners walifunga magoli matatu ndani ya dakika 16 za kipindi cha pili na kuibuka na ushindi huo.Magoli ya Arsenal yalifungwa na Bukayo Saka dk(53), Gabriel Martinelli dk(58) na Eddie Nketiah dk(69). 


Msimamo wa Premier League

Arsenal walipata ushindi huo mbele ya kocha wao wa zamani Arsene Wenger. The Gunners wanaongoza msimamo wa ligi kuu kwa alama 40 baada ya mechi 15, alama saba mbele ya Newcastle United ambao wamecheza mechi 16. 


Arteta Afichua Mipango ya Arsenal Kusajili Wachezaji Januari
Post a Comment

0 Comments