Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga SC yatinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho: Club Africain 0-1 Yanga Sc

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Yanga SC imetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho kufuatia ushindi wa jumla wa bao 1-0 dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Timu hizi zilitoshana nguvu kwa sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla goli la Stephanie Aziz Ki kuibusha Young Africans kwenda hatua ya makundi ugenini.

Yanga walicheza kwa nidhamu kwa dakika zote 90 huku wakiwa na utulivu wa hali ya juu,Kocha Nasreddine Nabi amechagua wachezaji sahihi wa kuanza nao jambo ambalo limekuwa faida kwa Yanga.

Walinzi wa Yanga walicheza kwa kutofanya makosa na kutowaruhusu Club Africain kutengeneza nafasi za wazi,Mlinda Mlango Djigui Diarra ameendelea kuwaweka Yanga salama dakika zote tisini. Amefanya save za maana katika mchezo wa leo.

Salum Abubakary alikuwa katika kiwango bora sambamba na Feisal Salum,Morisson ni mzoefu wa haya mashindano muda wote alikuwa akiwatuliza wenzake na mechi ikaonekana rahisi kwa upande wao.

Aziz Ki alikuwa na goli lake nje,nadhani usajili wake ulilenga hasa kuisaidia Yanga katika michuano ya Kimataifa. Mechi kubwa kama hii unahitaji wachezaji mwenye akili kubwa kama Aziz Ki.

Kuingia Yanga makundi ni faida kwa afya ya soka letu maana tunaweza tena kuingiza timu nne katika michuano ya Kimataifa msimu ujao.

HILI HAPAGOLI LA YANGA SC DHIDI YA Club Africain

Post a Comment

0 Comments