Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za soka Balani Ulaya Jumamosi tarehe 26.11.2022

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Manchester United wamefanya mazungumzo juu ya kumsajili tena mchezaji wao wa zamani raia wa Uholanzi Memphis Depay, 28, ambaye klabu yake ya sasa Barcelona ipo tayari kusitisha mkataba wake. (Sky Germany)

Chelsea na Real Madrid bado wapo katika mbio za kutaka kuinasa saini ya mshambuliaji kinda wa klabu ya Palmeiras Mbrazili Endrick despite wenye umri wa miaka 16 licha matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain kutangaza dau la mapema la kutaka kumnasa kinda huyo. (Fabrizio Romano)

Klabu ya Sampdoria ya Italia huenda ikasistisha mapema mkataba wa mkopo wa kiungo raia wa Uingereza Harry Winks anayemilikiwa na klabu ya Tottenham. Winks, 26 yupo katika mkopo wa mwaka mzima na Sampdoria lakini hajaichezea hata mechi moja klabu hiyo kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu. (Calciomercato - in Italian)

Kiungo raia wa Nigeria Alex Iwobi, 26, yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu unusu na klabu yake ya Everton utakaompatia mshahara wa £100,000 kwa wiki. (Sun)

Everton pia wapo tayari kuwaachia beki wa kati Mkolombia Yerry Mina, 28, na kiungo raia wa  Mali Abdoulaye Doucoure, 29, endapo watapata vilabu vya kuwasajili katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (GiveMeSport)

Ligi ya Primia haitatumia mwongozo mpya mkali wa Fifa juu ya dakika za majeruhi ambao umezifanya baadhi ya mechi katika Kombe la Dunia linaloendea nchini Qatar kuchezwa mpaka kwa dakika 100.   (Mail)

Manchester United wanapiga hesabu za kumnyakua mshambuliaji raia wa Ufaransa anayechezea klabu ya Bayer Leverkusen Moussa Diaby, 23. (Fichajes)

Bilionea Amancio Ortega, ambaye ni mmiliki wa maduka ya maarufu ya nguo na mitindo ya Zara hana mpango wa kuinunua klabu ya Manchester United licha ya ripoti za awali kumhusisha Tajiri huyo mwenye miaka 86 na ununuzi wa Mashetani Wekundu. (Cadena Cope - in Spanish)

Meneja wa Barcelona  Xavi Hernandez ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo mkabaji raia wa Uhispania Sergio Busquets mwenye miaka 34. (Sport - in Spanish)

Beki wa zamani wa Arsenal na Manchester City  Kolo Toure, 41, ameingia makubaliano ya miaka mitatu unusu kuwa kocha wa klabu inayoshiriki ligi ya Championship ya Wigan. (Football Insider)

Post a Comment

0 Comments