Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Richarlson Aiongoza Brazil Kuisambaratisha Serbia Katika Pambano La Kundi G

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

FOWADI Richarlson Andrade aliongoza Brazil kuanza vyema kampeni zao za Kundi G kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Serbia mnamo Alhamisi katika dimba la Lusail Iconic, Qatar.

Brazil wanaopigiwa upatu wa kunyanyua Kombe la Dunia mwaka huu, walisubiri hadi dakika ya 62 kufungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Richarlson ambaye ni mshambuliaji matata wa Tottenham Hotspur.

Bao hilo lilitokana na tukio la kipa Vanja Milinkovic-Savic kupangua kombora zito aliloelekezewa na Vinicius Junior. Richarlison alipachika wavuni bao la pili la Brazil kwa ustadi mkubwa baada ya kupokezwa krosi na Vinicius katika dakika ya 73.

Mabingwa hao mara tano wa dunia walimiliki asilimia kubwa ya mpira na kutamalaki mchezo huku Alex Sandro na Casemiro wakishuhudia makombora yao yakibusu mhimili wa goli la Brazil baada ya Fred kumwajibisha vilivyo Milinkovic-Savic.

Brazil walituma onyo kali zaidi kwa washindani wao kwa kuleta ugani Gabriel Jesus, Antony dos Santos na Gabriel Martinelli katika kipindi cha pili ili kudhihirisha utajiri mkubwa wa vipaji katika kikosi chao. Pigo la pekee kwa miamba hao wa Amerika Kusini ni jeraha lililomlazimisha nyota Neymar Jr kuondoka uwanjani akichechemea.

Serbia wanaoshikilia nafasi ya 21 kimataifa wangali na nafasi ya kutinga hatua ya 16-bora ikizingatiwa kwamba Uswisi waliopepeta Cameroon 1-0 wangali pia na kibarua kigumu dhidi ya Brazil wanaopigiwa upatu wa kutawala Kundi G.

Brazil wanaoshikilia nafasi ya kwanza kimataifa kimataifa, walitwaa Kombe la Dunia mnamo  1958, 1962, 1970, 1994 na 2002. Wameshiriki fainali za kipute hicho mara 22.

Post a Comment

0 Comments