Ticker

6/recent/ticker-posts

Makambo nje wiki sita

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Heritier Makambo atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita baada ya kugundulika amevunjika mfupa mdogo wa kifundo cha mguu.

Maneno hayo yamesemwa na Daktari wa Yanga, Moses Etutu kuwa vipimo vimeonyesha Makambo amepata jeraha hilo na itamchukua wiki sita kuwa nje ya uwanja akijiuguza.

“Alikuwa akilalamika sana kuwa anasikia maumivu makali akicheza, ikatulazimu kumfanyia vipimo na ikagundulika kuwa amevunjika mfupa mdogo kwenye kifundo chake cha mguu.

“Baada ya kugundua hilo tumemuanzishia ratiba ya matibabu ambayo inaweza kumchukua hadi wiki sita kuwa nje ya uwanja akiuguza jeraha lake,” amesema  Dokta Etutu.

kikosi cha Yanga kinatarajiwa kushuka dimbani  kesho Jumanne Novemba 22 mchezo  kucheza dhidi ya Dodoma Jiji na mchezo huo utakaochezwa saa 10:00 jioni katika uwanja wa Liti, Singida.

Post a Comment

0 Comments