Ticker

6/recent/ticker-posts

Kundi C: Argentina Na Poland Kukabiliana Kesho Jumatano

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 DOHA, Qatar


ARGENTINA ambao wanapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa mwaka huu 2022 watamaliza katika nafasi ya kwanza iwapo watashinda Poland kwenye mechi ya mwisho ya Kundi C, na kuongoza kwa pointi sita.

Baada ya kukumbana na kichapo cha 2-1 mbele ya Saudi Arabia katika mechi ya ufunguzi, vijana hao wa kocha Lionel Scolari walipata ushindi wa 2-0 dhidi Mexico, na kesho Jumatano watarejea uwanjani kwa mara ya mwisho kuwania nafasi ya kutinga hatua ya 16-Bora.

Kumbukumbu zinaonyesha timu hiyo kutoka Amerika Kusini inajivunia rekodi nzuri ya ushindi dhidi ya wapinzani wao baada ya kuibuka na ushindi mara sita dhidi mara tatu, pamoja na kutoka sare mara mbili.

Katika mechi ya Jumatano, Poland itategemea mchango mkubwa kutoka kwa mshambuliaji Robert Lewandowski aliyefunga dhidi ya Saudi Arabia, mechi ambayo kocha Czeslaw Mchiniewics aliamua kumpanga Arkadiusz Milik na Lewandowski kuongoza safu ya kutekeleza mashambulizi.

Kwa upande mwingine, Lionel Messi ambaye alifunga dhidi ya Mexico atapewa tena mzigo wa kuongoza kikosi cha Argentina, akisaidiwa na Enzo Fernandez aliyefunga bao la pili kwenye mechi hiyo.

Messi na jeshi lake wanapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi, lakini watakuwa wakikutana na timu ambayo ilionyesha kiwango cha juu dhidi ya Saudi Arabia ambao waliandikisha ushindi wa kihistoria kwa kutokea nyuma na kuibwaga Argentina.

Kabla ya kushindwa na Saudi Arabia, Argentina ilikuwa haijashindwa katika mechi 36, hivyo matokeo hayo ya Saudi Arabia yalitibua rekodi yao ya kutofungwa tangu Julai 2019, ilipochapwa 2-0 na Brazil katika nusu-fainali ya Copa Amerika.

Kadhalika hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Argentina kupoteza mechi ya kwanza katika fainali za Kombe la Dunia tangu 1990 ilipochapwa 1-0 na Cameroon, lakini ikafika fainalini na kuchapwa 1-0 na Ujerumani.

Katika mechi nyingine ya Kundi D mjini Lusail City, Saudi Arabia na Mexico zitakutana, kila moja ikipigania nafasi ya kufuzu kwa raundi ya 16-Bora.

Ni mechi ambayo Mexico watahitajika kushinda kwa mabao mengi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Post a Comment

0 Comments