Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Likizo Yatangazwa Saudi Arabia Kusherehekea Ushindi Dhidi ya Argentina

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  • Saudi Arabia imetangaza likizo ya kitaifa baada ya ushindi wa kihistoria dhidi ya miamba Argentina katika Kombe la Dunia  
  • Saudi Arabia ndio timu ya kwanza nje ya Bara Ulaya kuipiga Argentina katika Kombe la Dunia tangu Cameroon mwaka 1990 


Taifa la Saudi Arabia limetangaza Jumatano - Novemba 23 - kuwa likizo ya kitaifa baada ya ushindi wa kihistoria dhidi ya miamba Argentina katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar. 

Green Falcons walitoka nyuma na kusajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Argentina - matokeo ambayo sasa ni miongoni mwa yale ya kustaajabisha sana katka historia ya Kombe la Dunia. 

Nahodha Lionel Messi aliipa Argentina uongozi katika dakika ya kumi kwa mkwaju wa penalti na kilichofuata ni mabao matatu ya Albiceleste yakikataliwa katika kipindi cha kwanza kwa kuotea. 

Saleh Al-Shehri na Salem Al-Dawsari walipiga mabao ya haraka mwanzoni mwa kipindi cha pili na kuipa Saudi Arabia ushindi huo muhimu katika kundi C la Kombe la Dunia.

Matokeo hayo yalifikisha kikomo rekodi ya Argentina ya kucheza mechi 36 bila kupoteza hata moja - rekodi ambayo ilianza mwaka 2019. 

Kwa ushindi huo, Saudi Arabia ndio timu ya kwanza nje ya Bara Ulaya kuipiga Argentina katika Kombe la Dunia tangu Cameroon mwaka 1990. 

Kufuatia ukumbwa wa ushindi huu, ufalme wa Saudi Arabia umetangaza Jumatano kuwa likizo ya kitaifa kusherehekea ushindi huu mkubwa wa timu yao ya taifa. 


Post a Comment

0 Comments