Ticker

6/recent/ticker-posts

Fei Toto tupo tayari kuwakabiri Club Africain

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema wapo tayari kupambana na Club Africain na kupata matokeo yatakayowapeleka Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Young Africans itacheza ugenini Tunis-Tunisia leo Jumatano (Novemba 09) majira ya saa mbili usiku, ikiwa na deni ya kusaka ushindi wa aina yoyote ama sare ya mabao, ili ifuzu hatua ya Makundi.

Kiungo huyo amesema wamejiandaa vizuri tangu walipowasili Tunisia mwishoni mwa juma lililopita, hivyo watahakikisha wanapambana na kupata matokeo mazuri.

Hata Hivyo ‘Fei Toto’ amewahimiza Mashabiki wa Young Africans kuwa kitu kimoja na kuiombea timu yao kwa Mwenyezi Mungu, ili ifanikiwe kupata matokeo yatakayowapeleka hatua ya Makundi.

“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu ninawaomba mashabiki wote wa Young Africans kuendelea kutuombea kwani sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana kwa ajili ya kuwapa furaha, licha ya Presha ya mchezo huu ni kubwa.”

“Natambua kuwa tuna deni kubwa sana kwa watanzania na mashabiki wote, hivyo nasi tutapambana sana ili kuona timu ikicheza Hatua ya Makundi, tunaomba maombi pekee kutoka kwao.” amesema Fei Toto

Katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza hatua ya Mchujo uliopigwa jijini Dar es salaam Jumatano (Novemba 02), timu hizo zilitoka suluhu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Post a Comment

0 Comments