Ticker

6/recent/ticker-posts

Chama, Aziz KI wafungiwa michezo mitatu na Tff

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Nyota wa Simba, Clatous Chama na Stephane Aziz KI wa Yanga wamefungiwa kutocheza michezo mitatu na faini ya Sh 500, 000 (laki tano) kila mmoja.

Kufungiwa nyota hao ni kutokana na kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani katika mchezo wa Yanga na Simba uliopigwa Oktoba 23 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo miamba hiyo ilitoka suluhu.

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa uzingativu wa kanuni 41:5 (5.4) ya ligi kuu kuhusu uthibiti kwa wachezaji baada ya kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB) katika kikao chake cha Novemba 4 kupitia mwenendo wa matukio mbalimbali.

Katika michezo mitatu ambayo Chama ataikosa ni ule wa kesho dhidi ya Singida Big Stars Novemba 9, Ihefu FC Novemba 12 na Namungo Novemba 16.

Kwa upande wa Aziz KI ataikosa Kagera Sugar Novemba 13, Singida Big Stars Novemba 17 na Dodoma Jiji Novemba 22.

Michezo watakayoikosa Chama na Azizi Ki baada ya kufungiwa mechi 3


CHAMA πŸ‡ΏπŸ‡²                 AZIZ KI πŸ‡§πŸ‡«

1.Singida Big Stars.      1.Kagera Sugar 

2.Ihefu.                       2.Singida Big 

3.Namungo.                 3.Dodoma Jiji

Post a Comment

0 Comments