Ticker

6/recent/ticker-posts

Azam FC wataka alama tatu kutoka kwa Dodoma Jiji

Uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwenye mechi za ligi ambazo wanacheza kwa sasa wanahitaji pointi tatu tu na mabao kutoka kwa wachezaji wao.

Azam FC imetoka kuipa maumivu Simba kisha ikawatuliza Ihefu FC kwa dozi ya mwendo wa mojamoja kwa timu hizo huku mtupiaji wao akiwa ni Prince Dube.

 Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe alisema kuwa wanatambua ugumu uliopo kwenye kusaka matokeo lakini hilo haliwapi shida wanahitaji pointi tatu.

“Sisi ambacho tunakitaka kwenye mechi zetu ambazo tunacheza ni pointi tatu haijalishi tunacheza na mpinzani wa aina gani jambo la muhimu ni ushindi na mabao.

“Huwezi kupata pointi bila kufunga, wapinzani wetu tunawaheshimu na tunawafuata kwa tahadhari kubwa lakini ambacho tunahitaji ni pointi tatu,” amesema Ibwe.

Mchezo ujao wa Azam FC ni dhidi ya Dodoma Jiji unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex Novemba 9. huku kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya 3 ikiwa na pointi 17 baada ya kucheza mechi 9.

Post a Comment

0 Comments