Ticker

6/recent/ticker-posts

Mfahamu refa wa kike Mwafrika aliyechaguliwa kuchezesha Kombe la Dunia 2022

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Salima Mukansanga kutoka  Rwanda, aligonga vichwa vya habari baada ya kuingia kwenye vitabu vya historia kama mwanamke wa kwanza Mwafrika kuhudumu kama mwamuzi katika Kombe la Dunia la FIFA Qatar 2022 .

Kulingana na Mukansanga hakuwahi fikiria  kwamba siku moja atapata fursa kama hii adimu kuwa ama refa wa kike kwenye fainali za dimba la dunia. 

"Ilikuwa fursa ya kusisimua sana kwangu. Sijawahi kuwa na ndoto ya kwenda Kombe la Dunia la Wanaume," Mukansanga aliiambia FIFA.

"Kuteuliwa kwenye Kombe la Dunia la Wanaume ni jambo jipya, nafasi nyingine tunapata. Ina maana FIFA inatambua kuwa wanawake wanafanya kazi kwa bidii, tunatoa waamuzi wenye ubora na tunaweza kufanya kazi na kufika juu zaidi, hadi kileleni mwa mchezo wa wanaume. ." alisema Mukansanga.

Mwamuzi huyo tajika alipata ubabe mwingi alipokuwa mwamuzi wa mechi baina ya Zimbabwe na Guinea kwenye AFCON mnamo Januari 18, 2022.

Aliwahi ongoza timu ya wanawake kama Mwamuzi Msaidizi wa Video (VAR).

Licha ya Mukansanga kuchaguliwa kunao wengine kama vile Yoshimi Yamashita wa Japani na Mfaransa Stephanie Frappart walioteuliwa  pia kuwa marefa wa kike kwa mara ya kwanza kuchezesha Kombe la Dunia la wanaume.

Kwenye Michuano hii ya Kombe la Dunia la FIFA, Afrika itawakilishwa na nchi za Senegal, Cameroon, Tunisia, Morocco na Ghana.

Post a Comment

0 Comments