Ticker

6/recent/ticker-posts

Marefa 3 Wanawake Wanaopuliza Kipenga Katika Kombe la Dunia Nchini Qatar

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar ina waamuzi wa kati watatu wa kike - hii ikiwa mara ya kwanza kwa waamuzi wa kati wa kike kujumuishwa katika orodha ya waamuzi katika mashindano makubwa ya kimataifa.

Salima Mukansanga kutoka Rwanda 

Kamati ya FIFA kuhusu waamuzi ilimteua Salima Mukansanga raia wa Rwanda kuwa mmoaj wa marefa wanaoamua michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar. 

Mukansanga mwenye umri wa miaka 33 alikuwa mwaamuzi wa kati katika mechi ya kundi B kati ya Zimbabwe na Guinea katika mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) mnamo Januari 18, 2022 ambako Zimbabwe ilinyakua ushindi wa 2-1. 

Stephanie Frappart kutoka Ufaransa 

Stephanie Frappart ni refa wa pili mwanamke aliye na majukumu ya mwamuzi wa kati katika makala ya 22 ya michuano ya Kombe la Dunia. 

Mfaransa Frappart mwenye umri wa miaka 38 amekuwa na taaluma nzuri ya urefa, akiwa mwanamke wa kwanza kuwa refa wa kati katika mechi ya kombe la klabu bingwa Ulaya. 

Kando na kuamua mechi ya mataifa ua Ulaya kufuzu kombe la dunia, Frappart pia amekuwa mwamuzi wa kati katika mechi kadhaa za Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. 

Yoshimi Yamashita raia wa Japan 

Yoshimi Yamashita kutoka taifa la Japan anakamilisha orodha ya marefa watatu wa kike walio nchini Qatar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia. 

Yamashita alikuwa refa wa kwanza mwanamke kusimamia mechi ya kombe la klabu bingwa barani Asia mapema mwaka huu.

Wanawake watatu kuwa marefa wasaidizi 

Kando na marefa hao watatu, Kamati ya FIFA kuhusu Marefa pia iliwateua wanawake watatu kuhudumu kama marefa wasaidizi katika mashindano hayo. 

Watatu hao ni Neuza Back kutoka Brazil, raia wa Marekani Kathryn Nesbitt na mwenzake Karen Diaz Medina kutoka taifa la Mexico. 

Jumla ya marefa 36, marefa wasaidizi 69 na marefa wasaidizi wa video (VAR) 24 wako nchini Qatar kuamua michuano ya Kombe la Dunia. 


Post a Comment

0 Comments