Ticker

6/recent/ticker-posts

Kombe la Dunia: Senegal yaanza kwa kupoteza mechi ya ufunguzi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Timu ya taifa ya Senegal imelegeza kamba dakika za mwisho na kupoteza mechi yao ya ufunguzi katika Kombe la Dunia la mwaka 2022 nchini Qatar. 

Simba wa Teranga walinguruma kwa asilimia kubwa ya mchezo, wakitishia kurarua mpinzani wao Uholanzi na kumkaba kiasi kwamba alikosa shuti golini hadi dakika ya 84. 

Licha ya kutishia kutikisa wavu wa Uholanzi kwa makombora kadhaa, mabingwa hao wa mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) walishindwa wakitoka mchezoni bila goli. 

Uholanzi nayo ambayo ilifika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 na kulazwa na Uhispania 1-0 katika muda wa ziada, ilipata mabao yake na kushinda mechi hiyo 2-0. 

Mabao ya Uholanzi kwa mukhtasari Baada ya Senegal kutishia bila kupata lango la Uholanzi na kuwabana Oranje kiasi cha kukosa shuti la goli hadi dakika ya 84, vijana wa Louis van Gaal walichomoa mundu. 

Kiungo wa Barcelona Frenkie De Jong alipaisha mpira kwenye kisanduku katika dakika ya 84 na winga wa PSV Eindhoven kupiga goli la kichwa. 

Katika dakika ya tisa ya ziada, Memphis Depay aliachia kombora lililotemwa na kipa wa Senegal Edouard Mendy na Davy Klaassen kufunga bao la pili.

Post a Comment

0 Comments