Ticker

6/recent/ticker-posts

Kombe la Dunia Qatar 2022: Firmino afunguka kuachwa Timu ya Taifa ya Brazil

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mshambuliaji wa Klabu ya Liverpool Roberto Firmino amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutemwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Kocha Mkuu Adenor Leonardo Bacchi ‘Tite’ juzi Jumatatu (Novemba 07) alitangaza kikosi cha wachezaji 26, ambapo anaamini kitaweza kutetea Taifa la Brazil kwenye Fainali za mwaka huu.

Roberto Firmino amesema amesikia na kupokea kwa mikono miwili maamuzi ya mwisho ya Kocha ‘Tite’, hivyo atakuwa mtazamaji na kuiombea mema timu yake ya Taifa itakapokua Qatar.

Firmino amesema alitamani kuwa sehemu ya kikosi hicho kutokana na hitaji la kuitetea nchi yake, lakini anaamini ‘mambo hayakwenda’ kama alivyotarajia.

Amesema kuwa ‘hakuwaza’ kama angetemwa lakini hakuna sababu ya kulalamika zaidi anamshukuru Mungu na kuwapongeza walioteuliwa katika hiko kitakachoeleka Kombe la Dunia nchini Qatar.

“Mambo hayakwenda kama nilivyowazia au nilivyoota maisha yangu yote lakini natazama nyuma na nabaki kumshukuru Mungu kwa sababu tayari ameniruhusu kuishi ndoto hii mnamo 2018”

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wote walioitwa.” Ameandika Roberto Firmino katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Post a Comment

0 Comments