Ticker

6/recent/ticker-posts

Cristiano Ronaldo Atimuliwa Man United: "Atakiwa kuondoka Mara Moja"

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mshambuliaji matata Cristiano Ronaldo ametimuliwa katika klabu yake ya Manchester United baada ya uhusiano wake na miamba hao wa Uingereza kusambaratika kabisa. 

Kwa mujibu wa Manchester United, nyota huyo anaondoka klabuni humo mara moja baada ya kuafikiana makubaliano ya kuhimitisha ndoa yao kwa mara ya pili. 

Hii Imekuja siku chache baada ya mahojiano ambayo Ronaldo alitoa kwa Piers Morgan wakati akihojiwa katika kituo cha televisheni cha TalkTV, ambapo Mshambuliaji huyo aliikosoa vikali klabu hiyo.

Kupitia tovuti yao Man United wameandika kuwa "Klabu inamshukuru kwa mchango wake mkubwa katika vipindi viwili alivyokuwa Old Trafford, akifunga mabao 145 katika mechi 346, na inamtakia heri yeye na familia yake katika maisha mapya.

Baada ya taarifa hiyo Ronaldo amejibu kwa kusema:

“Kufuatia mazungumzo na Manchester United tumekubaliana pande zote mbili kumaliza mkataba wetu mapema. Naipenda Manchester United na ninawapenda mashabiki, hilo halitabadilika kamwe. Walakini, inahisi kama wakati mwafaka kwangu kutafuta changamoto mpya.

"Naitakia timu mafanikio kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu na kwa siku zijazo."


Post a Comment

0 Comments