Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Yaungana na Klabu Zingine za Ulaya Zilizomaliza Msimu Bila Kupoteza Hata Mechi Moja

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Yanga ilishinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2021/222 na kukamilisha msimu bila kupoteza mechi yoyote 

Barani Ulaya zipo klabu kadhaa ambazo ziliitangulia Yanga kufanya makubwa haya, klabu ya Arsenal ikiwa mojayazo 

Makala haya yanapakua orodha ya klabu zilizomaliza misimu bila kupoteza hata mechi moja za ligi katika mataifa mbalimbali ya Ulaya

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Yanga walikamilisha msimu wa mwaka 2021/22 bila kupoteza mechi yoyote, wakifunga msimu kwa kuitandika Mtibwa Sugar 1-0 mnamo Jumatano, Juni 29. 

Denis Nkane aliwafungia Wananchi bao hilo katika kipindi cha pili katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga wakikamilisha msimu na taji ambalo lilikuwa limeenda kwa mahasimu wao Simba kwa miaka minne mfululizo.


AC-Milan – (1991–92) 

Chini ya ukufunzi wa Fabio Capello, AC Milan ilicheza mechi 34 bila kupoteza mechi yoyote. Kando na kushinda taji, timu hiyo ilicheza mechi 58 kati ya mwkaa 1991 na 1993 bila kutandikwa na yeyote. 


Arsenal – (2003-04) 

Chini ya mwalimu Arsene Wenger, Arsenal ilishinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza bila kupoteza hata mechi moja. Kwa mechi 38 walizocheza msimu huo, the Gunners walishinda mechi 26, kutoka sare 12 na kutopoteza mechi yoyote. 

Msururu wa kutopoteza mechi ulitishiwa mechi sita ndnai ya msimu, mshambuliaji wa Manchester United Ruud van Nistelrooy alipopoteza panalti katika muda wa majeruhi na mechi hiyo kuishia sare ya 0-0. 

Mwanzo wa mwaka mpya, Arsenal ilishinda mechi tisa kwa mpigo kujihakikishia nafasi ya kwanza. 


Juventus - (2011-12) 

Chini ya ukufunzi wa nahodha wao wa zamani na kipenzi cha mashabiki Antonio Conte, Juventus walimaliza msimu bila kupoteza mechi yoyote. Hii ikiwa rekodi katika ligi ya timu 20 nchini Italia. 

Walimaliza msimu kwa alama 84, alama nne mbele ya AC Milan na rekodi yao ya kutopoteza mechi yoyote ilithibitishwa siku ya mwishdo ya msimu walipoitandika Atalanta 3-1. 

Kwa jumla walishinda mechi 23, kutoka sare mara 15 na kutopoteza hata mechi moja. 


Celtic - (2016-17) 

Celtic ilishinda mataji yoye matatu msimu huo ya Scotland na kushiriki mechi 47 nchini humo bila kupoteza yoyote. Kwa hilo wakabandikwa jina the “Invincibles”. 

The Bhoys chini ya ukufunzi wa Brendan Rodgers, walimaliza msimu wa mechi 38 bila kupoteza mechi yoyote na kuwa timu ya kwanza katika ligi ya Scotland kumaliza msimu bila kutandikwa tangu Rnagers katika msimu wa 1898-99 (msimu huu ulikuwa na mechi 18 pekee). 


Rangers - (2020-21) 

Kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Aberdeen katika siku ya mwisho ya msimu, Rangers walikamilisha msimu bila kupoteza mechi yoyote na kuwa timu ya kwanza tangu Celtic msimu wa 2016/17 kufikisha alama 100. 

Chini ya jagina wa Liverpool Steven Gerrard, Rangers walishinda mechi zote 19 ugani kwao Ibrox, kushinda mechi 32 kwa jumla na kutoka sare sita. 

Hawakufungwa hata bao moja katika mechi 26 na kwa mechi 38 walizocheza, waliruhusu mabao 13 pekee. 


Yanga - (2021-22) 

Baada ya kubabidhiwa taji lao la 28 la ligi mnamo Jumamosi, Juni 25, Wanajangwani walikuwa tu na jambo moja lililosalia- kumaliza msimu bila kupoteza mechi yoyote. 

Chini ya kocha Nasreddine Nabi Yanga iliitandika Mtibwa Sugar 1-0 katika siku ya mwisho ya msimu. 

Wananchi walimaliza msimu kwa alama 71, alama 11 zaidi ya nambari mbili Simba. Yanga ilishinda mechi 21, kutoka sare nane na kutopoteza hata mechi moja.

Post a Comment

0 Comments