Yanga imemtangaza Andrey Mtine kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo wakimchomoa kutoka klabu kubwa ya TP Mazembe ya DR Congo, lakini taarifa za uhakika ni kwamba bosi huyo ameanza na Al Hilal.
Mtine ameanza kushusha hesabu zote zitakazoisadia Yanga kuwashangaza matajiri hao wa Sudan, ikiwemno mikakati ya kocha wa timu hiyo Florent Ibenge ambaye ni raia wa DR Congo.
Mtine anamjua vizuri Ibenge tangu akiwa anafanya kazi Congo, lakini msimu uliopita tu kocha huyo aliwafanyia umafia na kuwang’oa Mazembe dhidi ya RS Berkane aliyokuwa anaifundisha na kwenda kutwaa taji la Kombe la Shirikisho Afrika.
Mabosi wa Yanga wameshaanza kuchukua tahadhari zote na hesabu zote kutoka kwa Mtine, ambaye pia ameshaanza kuziangalia mechi zote mbili.
Yanga itaanzia nyumbani dhidi ya Al Hilal, Oktoba 8, kabla ya timu hizo kurudiana baada ya wiki moja nchini Sudan, na mshindi wa jumla atatinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 Comments