Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga kumekucha, mastaa watano warejea kikosini

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Benchi la ufundi la Yanga limepata ahueni baada ya mastaa wake watano kurudi dimbani kisawasawa.

Mastaa hao watano wa timu hiyo walioko kambini Kigamboni, jijini Dar es Salaam wamepona majeraha na sasa wameanza kukiwasha kujiandaa na mechi ya Azam FC Septemba 6.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison wakati akihojiwa amesema kwamba Yanick Bangala, Lucapel Jesus Moloko walioumia kwenye mechi ya Coastal Union wameanza mazoezi ya uwanjani huku Crispin Ngushi akianza na programu nyepesi.

Kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze alisema wanaendelea na mandalizi kwaajili ya kujiweka fiti na kwenye orodha hiyo wameongezeka Joyce Lomalisa na Lazarous Kambole.

“Timu inaendelea vizuri na mazoezi kila mchezaji anatambua muhimu wa michezo iliyoko mbele yetu. Tutakuwa na mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuikabili Azam FC na mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Kaze na kuongeza;

“Wachezaji wetu wapo kwenye ari nzuri hata waliokuwa na majeraha wamerudi mazoezini akiwemo Crispin Ngushi, Joyce Lomalisa na Lazarous Kambole wameanza mazoezi ya Gym kwaajili ya kurudisha utimamu wa mwili,”.

Kaze alisema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanatetea mataji yao yote wanayoyashikiria wanatambua ugumu wa mashindano ya ligi na kimataifa wanapoambana kuhakikisha wanaiweka sawa timu ili iendelee kuonyesha ushindani.

Msimu huu Yanga imeanza na ushindi kwenye mechi zote mbili za ugenini dhidi ya Polisi Tanzania kwa mabao 2-1 na kuichapa Coastal Union mabao 2-0 wakati Simba yenyewe imeshinda mechi mbili za nyumbani kwa kuifungaa Geita Gold mabao 3-0 na Kagera Sugar mabao 2-0.

Post a Comment

0 Comments