Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba ,Yanga jikazeni kimataifa -Waziri Mchengerwa

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amezipongeza timu za Simba na Yanga kwa kutinga kwenye michezo ya mtoano hatua ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika

Baada ya kutoa pongezi hizo, Waziri Mchengerwa ameziambia timu hizo zisiridhike na ushindi walioupata na badala yake zijipange kuleta kombe la CAF nchini Tanzania.

''Watanzania na wanachama wa Simba na Yanga  wanafurahi kuona wanafanya vizuri katika mashindano haya ambapo amefafanua kuwa Mhe. Rais pia anaipongeza timu hizo huku  kutoridhika na ushindi walioupata  na badala yake waendelee kufanya mazoezi zaidi ili kujinoa hatimaye timu hizo zingie fainali na kuweza kurejesha kombe nyumbani; amesema Mchengerwa.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kufanya uwekezaji katika michezo ili kuwasaidia wananchi kueluka na magonjwa hivyo kujenga afya zao.

Klabu za Simba na Yanga zimetinga hatua hiyo baada ya Simba kupata ushindi wa jumla wa mabao 4-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi wakati Yanga SC imepata ushindi wa jumla wa 9-0 dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini.

Simba itacheza dhidi ya Premiero De Agosto ya Angola Ugenini huku Yanga kuanzia nyumbani dhidi ya Mabingwa wa Sudan Al-Hilal Omdurman, zote Oktoba 8, 2022.

Post a Comment

0 Comments