Ticker

6/recent/ticker-posts

Moses Phiri ‘na bado, nitafunga sana’

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

NYOTA wa Simba Mzambia Moses Phiri ametamba ataendelea kutupia sana, kwani ndio kazi yake. 

Phiri amefunga mabao manne katika mechi nne za kimashindano, zikiwamo tatu za Ligi Kuu Bara na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mwenyewe ameweka wazi kuwa hicho ndicho kilichomleta Msimbazi.

Mshambuliaji huyo juzi alifunga bao la kwanza katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets kabla ya nahodha John Bocco kutokea benchi na kufunga bao la pili lililowapa Simba ushindi wa mabao 2-0 ugenini.

Phiri amesema “Hata huko nilikokuwa (Zanaco) nilifunga ndio maana Simba ikaniona na kunisajili kwa sababu hiyo hivyo nahitaji kufunga zaidi na kuifanya timu ifikie malengo kwani ndicho kitu kilinileta hapa,”.

Phiri ni mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa na Simba msimu huu akitokea Zanaco ya kwao Zambia alikomaliza ligi na mabao 14 na msimu mmoja nyuma aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu Zambia akicheka na nyavu mara 16.

Ubora wa Phiri unazidi kuiimarisha safu ya ushambuliaji ya Simba inayoundwa na yeye, Dejan Georgijevic, Habib Kyombo na Bocco.


Post a Comment

0 Comments