Ticker

6/recent/ticker-posts

Mashabiki wa PSG wamemshutumu vikali Kylian Mbappe, Wamtaka Aaache ubinafsi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

MASHABIKI wa klabu ya Paris Saint-Germain wamemshutumu vikali mshambuliaji Kylian Mbappe kutokana na tabia yake ya ubinafsi.

Wamedai kwamba Mfaransa huyo amekuwa akikaa na mpira kwa muda mrefu badala ya kuwaandalia wenzake, hata wanapokuwa katika nafasi nzuri ya kufunga bao.

Kutokana na tabia hiyo, mashabiki hao wamemtaja kuwa mbinafsi hata rohoni mwake, tabia ambayo wamedai imeathiri uchezaji wa kikosi hicho kizima cha kocha Christopher Galtier.

Uchezaji wake Jumapili dhidi ya Olympique Lyon ambako PSG iliibuka na ushindi wa 1-0 haukufurahisha wengi na hadi sasa mashabiki wanazidi kutoa foka za kila aina kumshutumu mshambuliaji huyo.

Wamemlaumu kwa kukosa kuwaandalia wenzake mpira, hasa rafikiye Hakim Ziyech ambaye alikuwa katika nafasi nzuri ya kufunga.

Badala yake Mbappe ambaye alikuwa kwenye kikosi cha timu ya Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la 2018 aliendelea kuchenga na baadaye kuupoteza mpira.

Mbappe ni kati ya washambulaji matata na anaorodheshwa katika orodha ya wakali kama Robert Lewandowski, Karim Benzema na Erling Haaland.

Tayari mastaa hao wameonyesha ubora wao kwenye mechi za Klabu Bingwa barani Ulaya, na katika ligi za nyumbani.

Mbappe aliifungia PSG mabao yote mawili kwenye ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Jeventus, wakati Benzema akiongoza kikosi cha Real Madric kilichoibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Celtic.

Kuhusu Haaland, amekuwa moto wa kuotea mbali tangu ajiunge na Manchester City ambapo amekuwa akifungia katika kila mechi.

Alifunga mara mbili Manchester City iliposhinda Seville 4-0, wakati Lewandowski akipachika wavuni matatu akiwa na Barcelona dhidi ya Viktoria Plzen katika ushindi wa 5-1.

Wakati huo huo, kocha Mikel Arteta amesema aliamua kumpa kinda Ethan Nwaneri nafasi katika kikosi mnamo Jumapili baada ya chipukizi huyo kuonyesha kiwango kizuri mazoezini. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 15 aliisaidia Arsenal kushinda mechi hiyo 3-0, ugenini dhidi ya Brentford.


Post a Comment

0 Comments