Ticker

6/recent/ticker-posts

Man Utd 'kupunguza bajeti ya Usajili mwezi Januari'

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Manchester United wanatarajia kupunguza bajeti kwaajili ya Usajili wa mwezi Januari huku kukiwa na taarifa kwamba klabu hiyo imetumia kiasi kikubwa cha fedha katika usajili uliopita wa majira ya joto.

United walitumia karibu pauni milioni 200m katika dirisha la kwanza la usajili la kocha Ten Hag kuwasajili Casemiro, Tyrell Malacia, Lisandro Martinez, Christian Eriksen, Antony na Martin Dubravka, huku wao wakiingiza kiasi cha  pauni milioni 10m baada ya kumuuza Andreas Pereira kwenda Fulham.

Viongozi wa klabu hiyo walikuwa na nia ya kumuunga mkono Ten Hag, ambaye hivi karibuni alikiri kwamba anataka United ianze 'kujitayarisha kwaajili ya dirisha la mwezi Januari' ili kuendelea kusajili wachezaji wapya ili kuijenga timu anayo itaka, lakini kwa kanuni za fifa hilo swala halito wezekana.

United walikuwa wamepanga kutumia takriban kiasi cha pauni milioni 100 tu wakati wa dirisha la kwanza la usajili la kocha Ten Hag lakini wamejikuta wakitumia zaidi ya kiasi hicho katika usajili wa msimu huu wa majira ya joto.

Mmiliki wa United Joel Glazer, mtendaji mkuu Richard Arnold na mkurugenzi wa michezo John Murtough wote kwa pamoja wanapanga kutumia msimu wa mwaka 2023 katika majira ya joto, kama fursa ya kweli ya kuimarisha kikosi hicho.

United wanatarajia kumruhusu Ten Hag kuangalia uwezekano wa kuuza wachezaji kadhaa ambao tayari wanakabiliwa na mustakabali usio na uhakika ndani ya kikosi hicho, wakiwemo Phil Jones, Aaron Wan-Bissaka, Brandon Williams, Donny van de Beek na Cristiano Ronaldo ili kuweza kupata kiasi che fedha kwajili ya kuimarisha kikosi hicho msimu ujao.


.



Post a Comment

0 Comments