Ticker

6/recent/ticker-posts

KOCHA MAN UTD AWAHOFIA ARSENAL

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag ameonesha kutambua ukubwa wa Arsenal wakiwa wanaongoza ligi mpaka sasa wakiwa na alama 15.

Ten Hag alisema kuwa mechi ya Jumapili itakuwa ngumu sana na anatarajia kila mchezaji kwenye kikosi awe tayari kutekeleza jukumu lake uwanjani.

“Nimewona Arsenal, mpinzani ni mgumu, wameanza vizuri kama tunavyojua msimu huu, na unaweza kuona kuna timu ambayo iko pamoja kwa muda mrefu, ikiwa na kocha ambaye analeta falsafa yake kwenye timu.

“Kwa hivyo, huu ni mtihani mzuri na ninautazamia kwa hamu. Tutachagua kikosi sahihi kuanza lakini kama unavyoona, si timu pekee, tuna kikosi na pia, wachezaji waliojiunga nasi walifanya vizuri sana kwa hivyo nimefurahishwa na hilo.

“Hilo ndilo tunalopaswa kujenga zaidi.” Alimalizia Ten Hag

Manchester United watawakaribisha Arsenal kwenye mechi ya mzunguko wa sita, ambapo mechi hiyo itapigwa katika dimba la Old Trafford.

Post a Comment

0 Comments