Ticker

6/recent/ticker-posts

Kisinda amuondoa Kambole Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

YANGA imetengeneza mfumo mpya chini ya Rais wake, Mhandisi Hersi Said ambapo mastaa wao wanaopata shida wanawasaidia kila kitu, huku wakiwalipa mishahara na haki zao zingine ikiwamo bima za afya na posho.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, licha ya kumuengua Yacouba katika orodha ya mastaa wao msimu huu, bado wapo naye kikosini ambapo anafanya mazoezi na akiendelea kuonyesha kiwango bora kumshawishi kocha Nabi.

Ukiachana na Yacouba ambaye sifa yake ni kasi, lakini Mzambia Lazarous Kambole aliyesajiliwa hivi karibuni ameondolewa kwenye usajili kumpisha Tuisila Kisinda anayetarajiwa kutua muda wowote na klabu itaendelea kuwa nae na kumlipa stahiki zote lakini hatatumika kwani Yanga tayari ina wachezaji 12 wa kigeni.

Kambole ambaye amesajiliwa kutoka Kaizer Chiefs hajapata nafasi ya kuitumikia timu hiyo kwenye mechi za mashindano kutokana na kupata majeraha kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Namungo mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Avic Town Kigamboni.

Chanzo cha kuaminika kutoka kwenye uongozi kilisema kwamba wachezaji hao ni muhimu kwa Yanga na wanafikiria lolote linaweza kutokea kabla ya usajili wa Krisimasi. Wachezaji walioko kwenye hatari ya kuwapisha Kambole na Yacouba kwenye dirisha hilo ni Lucapel Moloko na Makambo ambao wanamulikwa kwa karibu sana na Nabi.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Saad Kawemba, alisema ni lazima sheria ifuatwe hivyo wachezaji waliowasajili ni mali ya Yanga lakini kati yao hao 14 wawili watabaki kuwa mali ya timu na 12 wamesajiliwa.

“Wote waliopo ni mali ya klabu wataendelea kuwepo watahudumiwa na klabu na wataendelea kuwepo kikosini,”alisema Kawemba ambae aliwahi kuwa kiongozi wa TFF, Mtibwa na Azam kwa nyakati tofauti.

Post a Comment

0 Comments