Ticker

6/recent/ticker-posts

Kipchoge avunja rekodi ya dunia Berlin


MWANARIADHA wa kimataifa wa Kenya, Eliud Kipchoge amevunja rekodi ya dunia ya marathon mjini Berlin ambayo aliiweka miaka minne iliyopita.

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 37 alivuka mstari kwa muda wa saa 2:01.09 katika mji mkuu wa Ujerumani na kuvunja rekodi aliyoweka katika mji huo huo kwenye mashindano hayo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kipchoge amevunja alama hiyo ya saa mbili hapo awali, akifanya hivyo mjini Vienna mwaka 2019, ingawa hilo halikutambuliwa rasmi kutokana na kutokuwa katika mashindano ya wazi.

Bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki pia alitumia timu ya kuzungusha pacemakers wakati wa mbio hizo za Vienna.

Kipchoge alifikia nusu ya kwanza kabla ya ratiba kwa dakika 59 na sekunde 51, lakini akapunguza kasi kidogo wakati wa nusu ya pili ya mbio hizo.

Ushindi huo unamaanisha kuwa Mkenya huyo sasa ameshinda marathon 15 kati ya 17 zikiwemo nne mjini Berlin na kusawazisha rekodi ya muda wote ya Haile Gebrselassie.

Mwenzake Mark Korir alimaliza wa pili kwa Kipchoge, huku Muethiopia Tadu Abate akikamilisha tatu bora.

Katika mbio za wanawake, Tigist Assefa wa Ethiopia aliibuka mshindi kwa muda wa dakika 2:15.37, ikiwa ni muda wa tatu wa kasi zaidi katika historia.

Post a Comment

0 Comments