Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea Kumuuza Romelu Lukaku Kupata Pesa za Kumnunua Harry Kane

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Chelsea wanajiandaa kumsajili mshambuliaji nyota wa Tottenham Hotspur Harry Kane msimu ujao wa joto. 

Blues wanataka Harry Kane kujiunga na kocha wao mpya Graham Potter ambaye ni shabiki mkubwa wa nahodha huyo wa Three Lions. 

Klabu hiyo itajaribu kufanya biashara na mahasidi wao wa London ambapo Romelu Lukaku atashuhudiwa akijiunga na Spurs. 

Lukaku bado ni mchezaji wa Chelsea na kwa sasa anachezea Inter Milan kwa mkopo.

Mbelgiji huyo alitia saini mkataba wa miaka mitano na Chelsea alipojiunga nao msimu uliopita hata hivyo, alitofautiana na kocha Thomas Tuchel na kulazimika kurejea Milan. 

Chelsea sasa wanataka kumtumia kuvizia Spurs kumwachilia Kane. The Sun linaripoti kuwa klabu hiyo inayomilikiwa na Todd Boehly itampeana Lukaku pamoja na pesa ili kupata saini ya Kane. 

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Spurs hawatakuwa tayari kufanya mazungumzo na Chelsea kumuuza mchezaji wao bora. 

Nahodha huyo Muingereza kwa sasa yuko na hadi 2024 kwenye mkataba wake na kuna uwezekano kwamba anaweza kushindwa kuurefusha. 

Wakati huo huo Bayern Munich tayari wametoa ofa kwa Kane huku wakimtaka kuwa kizibo wa Rober Lewandowski, ambaye alihamia Barcelona. 

Uhusiano wa karibu wa meneja wa Spurs Antonio Conte na Lukaku pia unaweza kuchochea ofa hiyo ya Chelsea, lakini Lukaku anafurahia kuwa Milan. 

Vile vile kuna mpango wa Lukaku kurefusha mkataba wake wa mkopo kwa mwaka mmoja zaidi huku vilabu hivyo viwili vikiendelea kujadili mkataba wa kudumu. 

Boehly alionyesha katika dirisha lake la kwanza la uhamishon kwamba yuko tayari kuvunja benki kusajili wachezaji visiki kwa klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments