Ticker

6/recent/ticker-posts

Beki Simba ataka aliyemleta Zoran ajiuzulu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

BEKI wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Daud Salum, amesema Simba isiishie tu kuvunja mkataba na Kocha Mkuu, Zoran Maki, badala yake imbane mtu aliyemleta kocha huyo.

Beki huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki fainali za Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria, amesema ufike wakati Simba ikafanya mambo yake kisasa.

“Huyu ni kocha wa ngapi anaondoka Simba katika muda mfupi? Aliyemleta ni nani? Yeye wakati anamtafuta huko hakufanya kazi yake ipasavyo, hivyo anatakiwa awajibike kwa hilo.

“Kama ni kiongozi wa kuchaguliwa ni vizuri akajiuzulu mwenyewe, kama ni mtendaji wa kuajiriwa awajibike mwenyewe, au mamlaka ichukue hatua.

“Ni aibu katika muda mfupi mnafukuza makocha karibu watatu, ina maana kuna watu hawafanyi kazi zao vizuri, wanapowatafuta huko, hapo ndipo yataibuka maswali mengi, yasiyo na sababu,” alisema.


Post a Comment

0 Comments