Ticker

6/recent/ticker-posts

Barcelona yaanza mchakato kutafuta mrithi wa Busquets

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya FC Barcelona imeaanza mchakato wa kutafuta mrithi wa kiungo wake mkabaji Sergio Busquets mwenye umri wa miaka 34 anayetajwa kuwa ataondoka klabu hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuwa ameitumikia klabu hiyo kwa miaka 17.

Wachezaji wanao tajwa kuwa FC Barcelona imewaorodhesha kuwa mbadala wa Busquets ni kiungo wa Wolverhampton Wanderers ya England Ruben Neves na Martin Zubimendi wa Real Sociedad ya Hispania. Dau la kumsajili Neves bado halijajulikana lakini mkataba wa Zubimendi unaonyesha anaweza kuondoka Sociedad kwa dau la Euro million 60 ambayo ni zaidi ya Bilioni 139 na milioni 452 kwa pesa ya Tanzania.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Hispania zinadai kuwa Sergio Busquets atajiunga na moja ya timu ya Ligi ya Marekani Major League Soccer. Busquets ameichezea FC Barcelona kwa misimu 15 kwenye timu ya wakubwa na miaka 2 kwenye timu ya vijana.

kwa ujumla ameichezea michezo 710 na amefunga mabao 10 tu na ameshinda mataji 30 ikiwemo ubingwa wa Ligi kuu Hispania La Liga mara 8 na ubingwa wa klabu bingwa Ulaya mara 3.

Post a Comment

0 Comments