Ticker

6/recent/ticker-posts

FT: YANGA 5-0 ZALAN FC .....MAYELE APIGA HAT-TRICK TENA.....AZIZ KI AENDELEA ALIPO ISHIA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KLABU ya Yanga SC imetinga raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Zalan FC kutoka Sudan Kusini mchezo wa  mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa katika uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza timu zote zilienda mapumziko bila kufungana huku Yanga wakiwa wameutawala mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulishambulia lango la Zalan FC kwa kasi na mnamo dakika ya 47 ya mchezo winga Farid Mussa alianza kufungua ukurasa wa mabao kwa kufunga bao safi la kuongoza.

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Stephanie Aziz Ki aliwanyanyua mashabiki wa Yanga dakika ya 56 akifunga bao la pili baada ya kuachia shuti lililomshinda mlinda mlango wa Zalan FC na kwenda moja kwa moja nyavuni.

Mshambuliaji hatari kwa sasa Fiston Mayele amepiga hat-trick yake ya pili baada ya kufunga mabao dakika ya 59,62 na 66,ikumbukwe mchezo wa kwanza Mayele alipiga hat-trick pia.

Kwa ushindi huo Yanga wametinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 9-0 baada ya mchezo wa kwanza kushinda mabao 4-0 na wanamsubiri mshindi kati ya St.George ya Ethiopia au  Al Hilal Omdurman kutoka Sudan.

Wawakilishi wengi katika Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Kipanga kutoka Zanzibar imetinga hatua ya raundi ya kwanza baada ya kushinda kwa Penalti 5-4 dhidi ya Al Hilal Wau.

Licha ya  Geita Gold FC kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Sahil wameshindwa kufuzu raundi ya kwanza kwa bao la ugenini badaa ya mechi ya kwanza kufungwa bao 1-0.

MAGOLI YOTE YANGA DHIDI YA ZALAN FC

Post a Comment

0 Comments