Ticker

6/recent/ticker-posts

Mfahamu Ethan Nwaneri mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza katika EPL

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Ethan Nwaneri mwenye umri wa miaka 15 amekua mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya ligi ya Uingereza kwenye mchezo wa ushindi wa 3-0 wa Arsenal dhidi ya Brentford.

Kiungo mshambuliaji wa Uingereza, ambaye alizaliwa Machi 2007, alichukua nafasi ya Fabio Vieira kwa washika mitutu wa London dakika za lala salama kwenye Uwanja wa Brentford Community.

Akiwa na umri wa miaka 15 na siku 181, Nwaneri alishinda rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Harvey Elliott.

Kiungo wa kati wa Liverpool Elliott alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 30 alipoichezea Fulham mnamo 2019.

Nwaneri alichukua nafasi ya Vieira, ambaye alikuwa amefunga bao la tatu, baada ya dakika 91 na sekunde mbili. Alihusika kwa dakika tatu na sekunde 42 kabla ya mchezo kumalizika baada ya dakika 94 na sekunde 44.

Ndiye mchezaji wa kwanza chini ya umri wa miaka 16 kucheza kwenye Premier League.

"Tuna nafasi ya kuleta wachezaji wachanga," alisema meneja wa Arsenal Mikel Arteta kabla ya mchezo.

"Sisi tuna upungufu sana na fursa huja wakati masuala yanapotokea."

Nwaneri amecheza mechi kadhaa akiwa na wachezaji wa chini ya miaka 18 wa Arsenal na aliichezea England timu ya chini ya miaka-16 alipokuwa na umri wa miaka 14.


Nwaneri ni nani?

Nwaneri alizaliwa tarehe 21 Machi 2007 punde tu baada ya Uwanja wa Emirates, uwanja wa nyumbani ambao Arsenal walihamia baada ya kuondoka Highbury, ulifunguliwa mwaka 2006.Amevutia haraka wakati akiwa na The Gunners.Akiwa na umri wa miaka 14, aliweka alama yake ya kwanza kwa vijana wa chini ya miaka 18 kwa bao dhidi ya Reading na kufuatiwa na maonyesho kadhaa ya kuvutia macho.

Alitarajiwa kutumia msimu huu na Vijana wa U-18 lakini alipandishwa haraka hadi Vijana wa U-21.Mnamo tarehe 8 Agosti, alifunga katika ushindi wa 3-0 baada ya kuingia kama mbadala wa England katika mchezo wa Vijana wa U-17 dhidi ya Visiwa vya Faroe.

Majeraha ya nahodha Martin Odegaard na Oleksandr Zinchenko yalimfanya Arteta akose nafasi ya kiungo dhidi ya Brentford."Ilikuwa hisia safi," aliongeza kocha wa Arsenal alipoulizwa kuhusu wakati alipoamua kumtuma Nwaneri.

Mashabiki wa Arsenal sasa watakuwa na matumaini kwamba anaweza kuendeleza maendeleo yake na kufuata mastaa kama Emile Smith Rowe na Bukayo Saka ili kuwa nyota mchanga katika klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments