Ticker

6/recent/ticker-posts

Liverpool na Real Madrid bado wanamtaka kiungo wa Flamengo Joao Gomes

Liverpool na Real Madrid zote kwa pamoja bado zinaendelea na harakati za kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Joao Gomes, licha ya kinda huyo wa Flamengo kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na waajili wake wa sasa.

Gomes mwenye umri wa miaka 21 anachukuliwa kuwa kama mmoja wa chipukizi bora zaidi katika ligi kuu ya Brazil, hivyo vilabu vingi kutoka barani Ulaya vinahitaji huduma yake.

Real na Liverpool zote zimekuwa zikimfuatilia Gomes kwa misimu kadhaa lakini hawako peke yao, Borussia Dortmund, Atletico Madrid, AC Milan na Lyon nao pia wanahitaji huduma yake.

Licha ya kuhusishwa na taarifa hizo, Gomes amekubali kusaini mkataba mpya wa muda mrefu - utakao mwezesha kusalia Flamengo hadi mwaka 2027 baada ya waajili wake kukubali kumuongezea mshahara wake mara nne.

Mapema mwezi huu, Gomes alifanya Maswali na Majibu ya moja kwa moja kupitia mtandao wa Instagram ambapo aliulizwa kama angependa kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza, haswa Liverpool, na mchezaji huyo wa miaka 21 hakusita kuzungumzia suala hilo.

"Liverpool ni timu ambayo ningependa kuchezea," alisema. "Nina hamu kubwa ya kucheza. Kucheza katika Ligi ya Mabingwa ndio ndoto yangu kubwa katika soka.”

Post a Comment

0 Comments