Ticker

6/recent/ticker-posts

Haaland afunga tena, Man City wakishinda 3-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mabingwa wa England Manchester City wamepanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England EPL, baada ya kuinyuka Wolverhampton Wanderers mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Molineux. Sasa wanaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 2 dhidi ya Arsenal wanaoshika nafasi ya pili.

Mabao ya ushindi ya Manchester City yamefungwa Jack Grealish aliyefunga bao la kwanza kunako dakika ya kwanza ya mchezo, Erling Haaland akaifungia City bao la pili dakika ya 16 hili ni bao la 11 kwa Haaland kwenye michezo 7 ya Ligi na ndio kinara kwenye orodha ya wafungaji na bao la tatu amefunga Phil Foden.

Wenyeji Wolverhampton walimaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya mwamuzi Anthony Taylor kumuonyesha kadi nyekundu beki Nathan Collins dakika ya 33 baada ya kumchezea madhambi Jack Grearish. Kwa ushindi huu Manchester City inaongoza Ligi kwa alama 17 ikiwa ni tofauti ya alama 2 dhidi ya Arsenal wenye alama 15 wakiwa nafasi ya 2 lakini City wamecheza michezo 7 mchezo mmoja zaidi ya Arsenal.

Post a Comment

0 Comments