Ticker

6/recent/ticker-posts

Graham Potter Kurithi mikoba ya Thomas Tuchel Chelsea

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

GRAHAM Potter ndiye anayepewa asilimia kubwa ya kuwa kocha mpya wa Chelsea, kujaza nafasi ya Thomas Tuchel aliyetimuliwa jana Jumatano baada ya klabu hiyo kushindwa 1-0 na Dinamo Zagreb ya Croatia, Jumanne usiku kwenye mechi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Lakini taarifa ya Chelsea imesema kichapo hicho hakiwezi kuchukuliwa kama sababu kuu ya kutimuliwa kwa Tuchel, kwani timu hiyo imekuwa ikisuasua tangu msimu huu uanze, licha ya kutumia pesa nyingi kusajili wachezaji wapya.

Licha ya Tuchel kusaidia Chelsea kushinda mataji ya Klabu Bingwa, UEFA Super Cup na Club World Cup, Chelsea haijaonyesha dalili za kufanya vizuri chini yake msimu huu.

Kutokana na sababu hiyo, bwanyenye Todd Boehly na wamiliki wapya wa klabu hiyo wameamua kuagana naye, mapema kabla ya mambo hayajaharibika sana.

Klabu hiyo imeamua kutumia mtindo wa bwanyenye wa awali wa klabu hiyo, Roman Abramovich ambaye aliweka rekodi ya kuwatimua makocha walioshindwa kuleta ufanisi, kabla ya kuamua kuuza klabu hiyo mwaka 2021.

Kufuatia habari za hivi punde, mbali na Potter, makocha wengine wanaotajwa orodha ya kutwaa nafasi ya Tuchel pale Stamford Bridge ni Zinedine Zidane na Mauricio Potchettino.

Taarifa ya Chelsea ilisema: “Klabu ya Chelsea leo imeagana na kocha Thomas Tuchel. Kwa niaba ya wafuasi wote wa Chelsea, klabu ingependa kumpongeza na wasaidizi wake kwa juhudi zake alipokuwa usukani. Daima, jina lake litabakia katika historia ya klabu baada ya kuongoza timu kutwaa mataji ya Klabu Bingwa, Super Cup na Club World Cup alipokuwa hapa.”

“Wakati huu wamiliki wapya wanafikia miaka 100 tangu wanunue klabu hii, wamiliki hao wanaamini wakati wa kufanya mabadiliko umetimia. Maafisa wa kiufundi waliobakia klabuni wataendelea kunoa kikosi hadi kocha mpya atakapopatikana,” taarifa hiyo iliongeza.

“Hakutakuwa na habari nyingine kuhusu idara ya kiufundi, hadi kocha mpya atakapopatikana,” iliongeza.

Mara tu Tuchel alipotimuliwa, kuliibuka madai kwamba Potter na Pochettino ndio pekee waliokuwa mstari wa mbele kupata kazi hiyo.

Pochettino anafahamia kutokana na ujuzi wake wa miaka mingine baada ya kuandaa klabu kubwa nchini hapa na pia alipokuwa na Paris-Saint Germain (PSG) nchini Ufaransa, lakini Potter ametambulika kutokana na jinsi klabu yake ya Brighton & Hove Albion inavyozidi kung’ara kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Baada ya mechi sita, Brighton inakamata nafasi ya nne jedwalini, wakati Chelsea ikitosheka na nafasi ya sita, baada ya kushindwa mara mbili dhidi ya Leeds United na baadaye Southampton.

Awali, Potter amewahi kukataa kusajliwa na Everton, Tottenham miongoni mwa timu nyingine, na haijulikani iwapo atakubali kuajiriwa na Chelsea.

Post a Comment

0 Comments