Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal 2-1 Zurich: ARSENAL Yaanza kwa Kishindo Europa League

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

ARSENAL wameanza kampeni ya Europa League msimu huu kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya FC Zurich ya Uswisi mnamo Alhamisi usiku.

Arsenal waliwekwa kifua mbele na chipukizi matata raia wa Brazil, Marquinhos, katika dakika ya 16 baada ya kushirikiana vilivyo na Eddie Nketiah.

Zurich walisawazisha mambo kupitia kwa penalty iliyojazwa kimiani na Mirlind Kryeziu mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya Nketiah kumwangusha Ola Selnaes ndani ya kijisanduku.

Nketiah aliwarejesha Arsenal uongozini katika dakika ya 62 baada ya kukamilisha krosi safi aliyoandaliwa na Marquinho. Chini ya kocha Mikel Arteta, Arsenal kwa sasa wanajiandaa kuvaana na PSV Eindhoven ya Uholanzi katika pambano la pili la Europa mnamo Septemba 15, 2022 uwanjani Emirates.

Post a Comment

0 Comments