Ticker

6/recent/ticker-posts

ZORAN: Yanga inafungika Kirahisi subirini muone

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


ZIMEBAKIA siku chache kabla ya kuchezwa mechi ya ufunguzi wa msimu kati ya Simba dhidi ya Yanga, ambayo itapigwa Agosti 13, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Kocha Zoran Manojlovic Maki akisema wala hana presha kabisa na pambano hilo la dabi.

Simba ilikuwa kambini Misri kwa muda wa wiki tatu kufanya maandalizi wakati watani zao Yanga walibaki Dar es Salaam, Kigamboni Avic Town.

Kocha Zoran amefanya mahojiano maalumu na amefunguka mambo mengi, huku akiweka bayana anavyoujua ushindani uliopo baina ya timu hiyo ya Msimbazi dhidi ya Yanga na Azam FC, lakini akisisitiza yeye ni mtu wa mechi kubwa.

Kocha huyo pia alifunguka juu ya maandalizi ya msimu mpya na namna kambi ya Ismailia ilivyomsaidia kuweka mambo mengi kiufundi na anakuja kumalizia kazi jijini Dar es Salaam akianzia na Simba Day kisha Ngao ya Jamii akisisitiza licha ya Yanga kuonekana kali, lakini bado inafungika.


MAANDALIZI YA MSIMU

Kocha wa Simba, Zoran Maki amesema katika maandalizi hayo ya msimu ujao wachezaji pamoja na benchi la ufundi wamefanya kazi nzuri kulingana na vile vitu vya kiufundi walivyohitaji.

Zoran anasema walikuwa na mwanzo mgumu kutokana na ugeni wake ndani ya timu, ugeni wa wachezaji pamoja na ratiba ngumu ya mazoezi, ila baada ya muda kila kitu kimeenda sawa.

Anasema wamefanikiwa kucheza mechi za kirafiki na kuonyesha mwanga kwa timu yao hasa kwenye mechi hizo na wameweka malengo ya kufanya vizuri msimu ujao.

“Viongozi wamefanya kazi yao vizuri kwa kuileta timu mahala salama na sahihi na hata wachezaji wamepokea kile ambacho nilikuwa nahitaji.”


Zoran anasema baada ya kumaliza maandalizi watarudi Tanzania watacheza mechi moja ya kirafiki kisha ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

“Malengo ya kwanza ni kuondoa rekodi mbaya ya kupoteza mechi ya ufunguzi wa msimu,” anasema Zoran na kuongeza:

“Bahati nzuri msimu huu tunafungua tena msimu kwa kucheza na wapinzani walewale tumedhamiria kushinda ili kuchukua taji la kwanza kama malengo yetu yalivyo msimu huu na baada ya hapo tutaanza kujipanga kwa ajili ya Ligi Kuu Bara itakayoanza Agosti 17.

“Tumeafanya maandalizi ya kutosha dhidi ya Yanga. Nimeangalia baadhi ya mechi zao na kufahamu udhaifu wao na kuna vingine tunavifanyia kazi ili kuhakikisha tunashinda mechi hiyo ngumu moja ya dabi kubwa Afrika.

“Kuhusu Ligi ya Tanzania ni ngumu na tunatakiwa kuanza kwa nguvu ili kumaliza vizuri kwani hii ni kama marathoni, kuhusu Kombe la Shirikisho (ASFC) nalo tutaandaa mipango yake kulingana na mechi zitakavyokuwa ili kuhakikisha tunafika fainali na kulibeba kombe hilo.”


Post a Comment

0 Comments