Ticker

6/recent/ticker-posts

Zoran Simba bado haijapata muunganiko mzuri.....asifu viungo washambuliaji

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

BAADA ya kuiongoza timu yake kupata ushindi katika mechi ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki, amekitazama kikosi chake kilivyocheza na kukili kwamba bado hakijapata muunganiko mzuri.

Simba juzi iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold FC, katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, shukrani kwa Agustine Okrah, Moses Phiri na Clatous Chama waliocheka na nyavu katika mechi hiyo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Zoran alisema kipindi cha kwanza wapinzani wao walicheza kwa kuzuia sana na alifanya mabadiliko baada ya kuona mapungufu yao na kuingiza mbinu za kuweza kupata matokeo.

Alisema mbinu zake zilifanikiwa, hivyo anawapongeza wachezaji wake kwa kupambana kwa sababu kisaikolojia hawakuwa sawa kutokana na mechi iliyopita.

“Mechi ilikuwa ngumu sana hasa kwa upande wa kisaikolojia baada ya kufungwa na Yanga, tulitengeneza nafasi katika kipindi cha pili na kupata mabao mawili, si rahisi hasa kuwa na wachezaji wengi wapya, lakini tunaendelea kuimarika,” alisema Zoran.

Alisema katika kipindi cha pili alifanikiwa kutawala mchezo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao tatu na pointi tatu muhimu katika mchezo wa kwanza.

“Kuhusu muunganiko wa wachezaji wangu, kwa sasa ni mapema kwa sababu wachezaji wengi ni wapya na tunaendelea kufanyia kazi kwa kila mmoja kupata nafasi ya kuweza kupata muunganiko mzuri na kupata kombinesheni,” alisema Zoran.

Alisema ubora wa safu yake ya kiungo cha ushambuliaji iko vizuri kwa uwezo ulionyeshwa na nyota wake wote akiwamo Okrah na Peter Banda.

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Geita Gold FC, Mathias Wandiba, alisema mechi ilikuwa nzuri na ushindani mkubwa kwa sababu walifanya makosa na Simba kuyatumia kupata ushindi.

Alisema kikubwa wameona mapungufu yao na wamekosa matokeo katika mchezo wa jana kwa sababu wachezaji wao hawakuwa makini na kufanya makosa ambayo Simba iliyatumia.

“Kimsingi Simba wametuzidi kwenye maandalizi ya msimu, lakini ndani ya uwanja tulikuwa 50 kwa 50 kwenye suala la kumiliki mpira, matokeo tu ndio yameangukia upande wao kwa kuwa walitumia nafasi,” alisema Wandiba na kuwapongeza Simba kupata matokeo mazuri lakini wachezaji wao kwa sababu ya kupambana na timu ambayo ifanya maandalizi mazuri ya msimu.


Post a Comment

0 Comments