Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Kuikabili Vipers Siku Ya Mwananchi..

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Yanga inatarajiwa kucheza dhidi ya Mabingwa wa Ligi ya nchini Uganda klabu ya Vipers katika kilele cha wiki ya Wananchi kinachotarajiwa kuwa Agosti 6, 2022.

Akiongea na waandishi wa habari Mjumbe wa kamati ya kuratibu wiki ya wananchi Taji Liundi amesema pamoja na mchezo huo lakini pia kutakuwepo na shughuli mbalimbali za ushereheshaji kutoka kwa wasanii mbalimbali wakubwa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa katika dimba la Benjamin Mkapa huku shauku kubwa ikiwa ni kushuhudiwa kwa mkali wa mabao wa klabu ya Vipers anayewindwa na wapinzani wao Simba, mshambuliaji Cesar Lobi Manzoki.

Aidha mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu wiki ya wananchi Arafat Haji amesema Taasisi ya fedha ya CRDB imeingia ubia na klabu hiyo kushirikiana nayo katika kufanikisha utekelezaji wa maadalizi na ufanisi wa wiki ya wananchi

Post a Comment

0 Comments