Ticker

6/recent/ticker-posts

"Simba, Yanga kuvaana Oktoba 23, 2022"

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


AGOSTI 13 mwaka huu ni mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba kuashiria uzinduzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini ikufikie rasmi sasa Oktoba 23, 2022 miamba hiyo itavaana katika mchezo wa duru la kwanza la ligi hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Almas Kasongo,  Simba itaanzia nyumbani ikiikaribisha Geita Gold Agosti 17, wakati bingwa mtetezi Yanga ataanzia ugenini kuivaa Polisi Tanzania, Agosti 16.

Amesema ligi hiyo itakayoanza Agosti 15 imezingatia mambo mbalimbali ikiwemo michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na mashindano mengine na kwamba Ligi Kuu msimu wa mwaka 2022/23 itamalizika Mei 27, mwakani.

Ratiba inaonesha kuwa Agosti 15, mwaka huu mechi za ufunguzi itakuwa Ihefu FC dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Highland State, Namungo FC  itaikaribisha Mtibwa Sugar, Uwanja wa Majaliwa, Lindi.  

Post a Comment

0 Comments