Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba yaizidi kete Yanga Kwa Manzoki

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KLABU ya Simba SC imeamua kutoa dau la dola 100,000 (Zaidi ya Milioni 230 za kitanzania) kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Afrika ya Kati Cesar Lobi Manzoki mwenye asili ya DR Congo kutoka klabu ya Vipers SC ya Uganda.

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye klabu ya simba imeamua kufanya kweli baada ya kukubali kulipa kiasi cha fedha za kigeni dola 100,000 kumngoa mshambuliaji Cesar Lobi Manzoki kutoka klabu ya Vipers SC ya Uganda.

Juzi viongozi wa Yanga walikwenda Uganda kujaribu kuingia makubaliano na timu ya vipers kuona kama kuna uwezekano wa kumpata Cesar Lobi Manzoki.

Timu zote mbili Yanga na Vipers walikuwa wameingia makubaliano kuhusu mchezaji huyo lakini Cesar Manzoki amekataa kwenda Yanga na kusema kuwa yeye ni mtu anayesimamia neno lake kwasababu alishasema atachezea Simba.

Na ameiambia timu yake ya vipers kuwa hawezi kuwaangusha timu ya Simba na kwasababu alikuwa tayari na makubaliano nao na anaipenda Simba.

Na ametueleza kuwa kwasasa kipaumbele chake ni Simba na atafikiria kwenda nchi nyingine lakini kwa Tanzania timu atakayo cheza ni Simba tu.Post a Comment

0 Comments