Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba SC kurejea nchini leo kuelekea ‘Simba Day’


KLABU ya soka ya Simba yenye makazi yake mitaa ya Msimbazi jijini Dar es Salaam Inatarajia kurejea nchini leo tarehe 4 Agosti, 2022, Ikitokea nchini Misri ilipokuwa imeweka kambi ya kujiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya NBC 2022/23 na mashindano ya kimataifa.

Klabu hiyo iliondoka nchini tarehe 14 Julai, 2022, ikiwa na msafara wa wachezaji 19, wengine wakikwama kwasababu ya maswala ya viza na wengine wakiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Aidha timu hiyo iliweka kambi Misri katika jiji la Ismailia na kucheza michezo minne ya kirafiki kwa ajili ya kupima kikosi chao kuangalia ubora na mapungufu.

Katika michezo hiyo minne waliyocheza waliweza kushinda michezo miwili,sare moja, na kupoteza mchezo mmoja na timu walizo fanikiwa kucheza nazo ni pamoja na Isimaila FC , AL-Kholood Club , Haras El Hodoud.

Aidha timu hiyo itarejea leo inchini kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day itakayofanyika tarehe 8 Agosti, 2022 katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Siku hiyo ni maalumu kwa ajili ya kutangaza kikosi chao chote na benchi la ufundi ambapo kuna mabadiliko na maingizo mapya pia watakuwa na maandalizi kwaajili ya mechi ya ngao ya hisani dhidi ya mtani wake Yanga itakayopigwa tarehe 13 Agosti, 2022 katika uwanja wa Mkapa

Post a Comment

0 Comments