Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba kucheza na mabingwa wa Ethiopia ‘Simba Day’

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KLABU ya soka ya Simba imetangaza rasmi kuwa itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya St. George ya Ethiopia katika maadhimisho ya tamasha la siku ya Simba ‘Simba Day’ katika dimba la Benjamin mkapa Jijini Dar es Salaam. 

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 5 Agosti, 2022 katika ukurasa rasmi wa klabu ya Simba wa Instagram.

Klabu ya St. George ambao ndio mabigwa wa ligi kuu ya Ethiopia itacheza na Simba katika tamasha hilo ambalo hutumika kutambulisha wachezaji pamoja na benchi la ufundi ambalo litaitumikia timu katika msimu mpya wa ligi kuu ya NBC na michuano mengine ikiwemo ya kimataifa.

Pia tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu litafanyika tarehe 8 Agosti, 2022, hutoa fursa kwa mashabiki na wapenzi wa Simba kuja kushuhudia timu yao kabla msimu mpya haujaanza.

Huu umekua utaratibu wa Klabu ya Simba kutoa mwaliko kwa timu za nje ya Tanzania kuja kushiriki nazo pamoja katika tamasha hilo ambapo katika msimu uliopita waliipa mwaliko klabu ya TP Mazembe kutoka nchini DR Congo na Simba waliweza kupoteza katika mchezo huo wa kirafiki.

Simba ambao walirejea nchini siku ya jana wakitokea nchini Misri walikuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao pia wana kibarua cha mechi ya Ngao ya jamii dhidi ya watani wao wa jadi klabu ya soka ya Yanga inayotarajiwa kucheza siku ya tarehe 13 Agosti 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Aidha timu hiyo bado inaendelea na usajili ili kuzidi kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao baada ya msimu uliopita kutokuwa mzuri kwao kwani walipoteza mataji yao yote matatu yaliyochukuliwa na mpinzani wao Yanga kuanzia ngao ya jamii , ligi kuu na kombe la Shirikisho la Azam.

Post a Comment

0 Comments