Ticker

6/recent/ticker-posts

Paula Kajala afunguka kuhusu mahusiano yake, sifa anazozingatia kwa mwanaume

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Mwanamitindo maarufu kutoka Bongo Paula Kajala ameweka wazi kwamba yupo kwenye mahusiano.

Katika mahojiano na Wasafi media, binti huyo wa muigizaji Kajala Masanja alifichua kuwa anachumbiana na jamaa ambaye hakutambulisha.

"Niko na mpenzi. Nipo kwenye mahusiano," Paula alisema Jumatano.

Kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja ambacho kimepita mwanamitindo huyo amedaiwa kuwa kwenye mahusiano na Rayvanny.

Hata hivyo alidinda kujibu ikiwa bado anachumbiana na staa huyo wa Bongo au moyo wake ulishatekwa na mwanaume mwingine.

"Sitaki kuongelea hilo, mtajua Ijumaa. Nitaongea sana, nitafichua vitu vingi," Alisema.

Rayvanny na Paula wanadaiwa uchumbiana kwa miezi kadhaa mwaka jana kabla ya tetesi kuzuka mapema mwaka huu kuwa wametengana.

Katika kipindi cha mahusiano yao wawili hao walipakiana kwenye mitandao ya kijamii na kuandikiana jumbe za mahaba. Hata hivo hilo halijajitokeza kwa miezi mingi sasa, dokezo kuwa wawili hao hawapo pamoja tena

Katika mahojiano ya Jumatano Paula alifichua sifa mbalimbali ambazo anazingatia  kwa mwanaume wa kuchumbiana naye.

"Napenda mwanaume mcha Mungu, awe mrefu, awe mrefu na  awe ananukia," Alisema.

Mwanamitindo huyo aliweka wazi kuwa mwanaume anayemdai ni sharti awe na hela na malengo ya kimaisha.

"Lazima awe tajiri. Awe mweusi, sipendi wanaume light skin na awe mwanaume ambaye anajielewa," Alisema Paula.

Wiki chache zilizopita, binti huyo wa Kajala aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa na kutimiza umri wa miaka 20.

Aprili mwaka jana, Paula alidaiwa kuhusika katika kuvunjika kwa mahusiano ya mamake na mchumba wake Harmonize.

Kajala na Harmonize waliripotiwa kutengana baada ya bosi huyo wa Konde Music Worldwide kuanza kumnyemelea Paula na hata kumtumia picha za uchi.

Hata hivyo, mwaka mmoja baadae wasanii hao wawili hatimaye walirudiana na hata wanapanga kufunga pingu za maisha hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments